Jumamosi, 18 Aprili 2015

Watu zaidi ya 30 wauawa Afghanistan

                                                         Eneo kulikotokea shambulizi     

  Shambulizi la kujitoa mhanga kwenye mji ulio mashariki mwa Afghanistan wa Jalalabad limewaua watu 33 na kuwajeruhiwa karibu wengine 100.
Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea karibu na benki ambapo wafanyakazi wa serikali wanalipwa misharaha yao.
Maafisa wamesema kuwa mtu aliyefanya  shambulio hilo alikuwa na pikipiki.
Kulitokea shambulizi la pili karibu na madhabahu mjini Jalalabad lakini haijajulikani kama kulikuwa na madhara yoyote.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika, lakini mji wa Jalalabad umekuwa ukilengwa kila mara na kundi la Taliban.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni