Uchunguzi wa chembechembe za DNA unatarajiwa kufanywa kwa mujibu wa maafisa wa nchini Iraq katika mwili wa Izzat Ibrahim al Douri ambaye ni mwanachama wa mwisho wa uliokuwa utawala wa Saddam Hussein ambaye amekuwa akitafutwa.
Maafisa wa jeshi wamesema kuwa aliuawa na vikosi vya serikali wakati msafara wake uliposhambuliwa karibu na mji wa Tikrit
Bwana al Douri anaaminika kuchangia pakubwa katika ukuaji wa kundi la Islamic State nchini Iraq.
Aliyekuwa msemaji wa chama cha Baath ambacho kilikuwa chama chake al - Douri alikana kuuawa kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni