Jumatano, 15 Aprili 2015

Watu 400 wafa maji wakielekea Italia

Kundi la wahamiaji manusura waliokolewa kutoka kwa bahari ya Mediterenia limewasili Italia


Kundi la wahamiaji manusura waliokolewa kutoka kwa bahari ya Mediterenia limewasili Italia.
Manusura hao walikuwa miongoni mwa wamiaji waliokuwa wakielekea bara Lla Ulaya kabla ya boti yao kuzama na kuua zaidi ya watu mia nne.
Manusura hao wamepokelewa katika kisiwa cha Sicily na maafisa wa usalama na wale wa uhamiaji waliowapiga picha na kuchukua majina yao.

            Manusura hao wamesajiliwa kisiwa cha Sicily

Awali Shirika la Umoja wa mataifa, lilitoa wito kwa juhudi zaidi zifanywe ili kuokoa maisha ya wahamiaji wanaojaribu kufika bara Ulaya kutokea Kazkazini mwa Afrika.
Zaidi ya wahamiaji 400 wanahofiwa kufa maji baada ya boti walilokuwa wakilitumia kuzama siku ya Jumatatu katika bahari ya Mediterenia.
Msemaji wa umoja wa mataifa anayejishughulika na wakimbizi Laurens Jolles amesema kuwa, juhudi za sasa za kujaribu kuwaokoa wahamiaji ni chache mno.

Manusura hao wamepokelewa katika kisiwa cha Sicily

Mwaka jana jumuiya ya bara Ulaya iliongeza operesheni ya uokoaji baharini, huku baadhi wakihoji kuwa huduma hizo zitachangia pakubwa idadi ya wahamiaji wanaovuka bahari na kuingia barani Ulaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni