![]() |
Wahamiaji waliokolewa siku ya Jumapili |
Nahodha wa mashua ambayo ilizama nje ya pwani ya Libya siku ya Jumapili ambapo mamia ya wahamiaji waliangamia amefikishwa mahakamani kwa makosa ya kuua.
Maafisa nchini Italia wanasema kuwa nahodha huyo raia wa Tunisia na mhudumu mwingine wa chombo hicho pia wameshtakiwa kwa kusadia uhamiaji ulio kinyume cha sheria.
Wawili hao walikuwa ni miongoni mwa manusura 27 ambao waliawasili katika kisiwa cha Sicily siku ya Jumatatu.
Wawili hao wanafunguliwa mashtaka wakati Muungano wa Ulaya unapotangaza mikakati ya kukabiliana na suala la uhamiaji katika bahari ya Mediterranean.
Kati ya hatua zilizotangazwa ni pamoja na kuwepo shughuli za kutafuta na kuokoa mashua huka pia kukiwa na kampeni ya kuharibu mashua zinazotumiwa kusafirisha wahamiaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni