Serikali ya Ukraine imesema kuwa waasi wanaoungwa mkono na Urusi wamekiuka pakubwa muafaka wa amani mara 20 zaidi.
Muafaka huo uliafikiwa kusitisha vita katika mji wa Donetsk ulioko mashariki mwa Ukraine.
Duru kutoka kusini mashariki mwa Ukraine, zinasema kuwa kumeshuhudiwa mapigano mapya kati ya wanajeshi waaminifu kwa serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
Mapigano yamezidi katika kijiji cha Shyrokyne - kilichoko katika mji wa bandarini wa Mariupol.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni