![]() |
Basi lasombwa na mafuriko |
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mandera kazkazini mwa Kenya wanasema kuwa takriban watu 16 hawajulikani walipo baada ya basi kusombwa na mafuriko kilomita chache kutoka mji huo.
Mvua kubwa iliripotiwa kunyesha katika eneo la mji huo na viunga vyake mapema siku ya alhamisi.
Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu Abbas Gulet amesema kuwa wamewaokoa watu 42 kufikia sasa.
Basi hilo liliondoka mjini Mandera likielekea jijini Nairobi mapema siku ya jumatatu kabla ya kukwama katika matope.
Baadaye mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kulisomba basi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni