![]() |
Diego Costa akianguka katikakati ya wachezaji wa stoke city |
Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha mshambuliaji Diego Costa baada ya kujeruhiwa wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-1 dhidi ya kilabu ya Stoke City siku ya jumamosi.
Costa alichukua mahala pake Oscar wakati wa mapumziko huku mabao yakiwa 1-1, lakini alicheza kwa dakika 10 pekee kabla ya kulazimika kutoka nje baada ya kupata jeraha jengine.
''Kama matokeo yangalikuwa 2-0 asingecheza.Lakini ilibidi tumchezesha .Kitengo changu cha matibabu kiliamua kumchezesha'', alisema Mourinho.
Amesema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa wiki mbili .
Hii inamaanisha kwamba Costa ataikosa mechi dhidi ya QPR tarehe 12 mwezi Aprili na ile dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 18 mwezi Aprili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni