Jumatatu, 20 Aprili 2015

Uchina kuwekeza mabilioni Pakistan


                                                 Bango la kumkaribisha rais Xi nchini Pakistan.
Rais wa China Xi Jinping ameanza ziara ya siku mbili nchini Pakistan hii leo.
Bw Xi atazindua mpango wa uwekezaji wa kichina wa gharama ya dola bilioni 50 ambao Pakistan ina matumaini kuwa utasuluhisha tatizo lake la nishati.
Mpango huo unaofahamika kama barabara ya uchumi ya China na Pakistan ni pamoja na barabara , reli na mabomba ya jumla ya umbali wa kilomita 3000 kutoka mji wa bandari wa Gwadar nchini Pakistan hadi mji wa ulio mashariki mwa China wa Kashgar.
Waandishi wa habari wamesema kuwa lengo la China ni kuongeza ushawishi wake wa kiuchumi kwa Pakistan ili kulegeza ule wa Marekani na India.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni