Viongozi wa Ulaya wanachagizwa kubadilisha namna wanavyokagua bahari ya Mediterranean baada ya maafa ya karibuni yaliyowakuta wakimbizi waliokuwa wakivuka kutoka Afrika.
Inahofiwa kuwa mamia ya watu wamezama baada ya mashua yao kwenda mrama nje ya mwambao wa Libya.
Mkuu wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, alisema hali ya sasa haikubaliki - na katika mkutano mjini Brussels Jumatatu, atapendekeza kuwa hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa.
Viongozi wa Malta na Utaliana wameonesha hasira kuwa nchi zao zimeachwa kubeba jukumu la msukosuko huo peke yao.
Juhudi za kusaka mashua na kuokoa wakimbizi zilipunguzwa mwaka jana kama njia ya kuwakatisha tamaa wakimbizi wasijaribu safari hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni