![]() |
Raia wa Armenia wakiwa katika kumbukumbu ya mauaji vita kuu ya dunia. |
Raia wa Armenia kutoka pande zote Duniani wamekusanyika mji mkuu wa Armenia Yerevan kufanya kumbukumbu ya mauaji ya watu milioni moja na nusu mjini Ottoman Uturuki katika vita ya kwanza ya dunia miaka 100 iliyopita.
Wakuu wa serikali wakiwemo Marais wa Urusi na Ufaransa wanatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu hizo ambazo wengi wanaziita kama mauaji ya kimbari ya Armenia.
Hata hivyo Uturuki inapinga kumbukumbu hizo ikidai kuwa mauaji hayo ni ya makundi mengi zaidi wakati huo wa vita hivyo na kwamba si Armenia pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni