Jumamosi, 18 Aprili 2015

Jacob Zuma aahirisha ziara ya Indonesia

                                                                Waandamanaji Afrika Kusini  


Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma ameahirisha ziara yake ya ughaibuni kutokana na hali ya ghasia za kibaguzi dhidi ya wageni katika taifa lake.
Rais Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano nchini Indonesia.
Polisi nchini Afrika Kusini wamewaagiza raia kutotuma ujumbe usiothibitishwa kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni kwa sababu hatua hiyo inazua hofu.
Polisi wamesema kuwa kuna wasiwasi kuwa uvumi huo unachochea ghasia dhidi ya wahamiaji.
                          Maafisa wa polisi wakikabiliana na waandamanaji Afrika Kusini
Watu 30 waliakamatwa wakati wa ghasia za usiku kucha mjini Johannesburg.
Biashara kadha zinazomilikiwa na raia wa kigeni ziliharibiwa.
Takriban watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yaliyaonza baada mfalme wa kizulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni wanahitajka kuondoka Afrika Kusini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni