Jumanne, 21 Aprili 2015

Mawaziri 16 waapishwa Afghanistan

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani


Baada ya miezi kadha ya mizozo ya kisiasa, rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amewaapisha mawaziri 16 wapya kwenye sherehe zilizofanyika mjini Kabul.
Hii inamaanisha kuwa baraza la mawaziri sasa limekamilika na nafasi ya waziri wa ulinzi imebaki wazi kufuatia kutoelewana kwa serikali ya umoja.
Wale wote walioteuliwa hawajashikilia nyadhifa kama hizo na wengi ni vijana na waliosoma na wanne kati ya mawaziri hao ni wanawake.
Kinyume na ilivyo kuwa awali, rais Ghani ameahidi kuwateua watu walio na ujuzi  .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni