Jumamosi, 25 Aprili 2015

Kijana aliyewavamia polisi auawa Israel

Maafisa wa polisi wa Israel



Polisi nchini Israeli wamesema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa na kisu kwenye kizuizi kimoja mashariki mwa Jerusalem.
Wamesema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 alijaribu kuwadunga kisu maafisa wa mpakani alipokuwa akiwavamia maafisa hao na kisu mkononi.
Kisa hicho kilitokea mapema jumamosi karibu na kizuizi cha Al-Zaim
Polisi wa Isreali walichapisha mitandaoni picha na kisu ambacho kijana hiyo alikuwa nacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni