Alhamisi, 23 Aprili 2015

Wahamiaji:Muungano wa Ulaya wapingwa

Waandamanaji wakipinga vifo vya wahamiaji wanaovuka bahari ya shamu kwenda Ulaya


Makundi ya kupigania haki za kibinadamu yamesema kuwa mikakati ilioafikiwa na muungano wa ulaya kuzuia idadi kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka hadi Ulaya kutoka Afrika sio ufumbuzi wa tatizo hilo.
Katika kikao cha dharura kilichofanyika mjini Brussels siku ya alhamisi, Viongozi wa Ulaya walikubaliana kuongeza msaada wao mara tatu ili kuimarisha usakaji na uokozi wa wahamiaji katika bahari ya shamu.
Pia waliidhinisha mikakati ya kukamata na kuharibu vyombo vinavyotumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao.
Lakini Shirika la Human Rights Watch pamoja na lile la kuwasaidia watoto la Save the Children, yamesema kuwa EU inafaa kuongeza juhudi zake katika uokoaji badala ya kulinda mipaka yake.
Mkutano huo uliitishwa baada ya zaidi ya watu 800 kupoteza maisha  weekend iliopita baada ya boti yao kuzama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni