Jumanne, 21 Aprili 2015

Jeshi kutuliza ghasia Afrika kusini

Waafrika kusini wakimpiga raia wa kigeni


Waziri wa ulinzi nchini Afrika kusini ametangaza kuwa jeshi litatumwa wakati ghasia dhidi ya wageni zikiwa zimesababisha vifo vya watu Saba.
Nasiviwe Mapisa-Ngqakula amesema kuwa ombi la kutumwa kwa wanajeshi liliamuliwa baada ya polisi kuomba msaada.
Hata hivyo hakusema ni wanajeshi wangapi watatumwa mitaani na jeshi litatumwa kwenda maeneo yanayoshuhudia ghasia nyingi ikiwemo mikoa ya Kwa Zulu Natal na Guateng.
Wakati wa ghasia kama hizo mwaka 2008 jumla ya watu 63 waliuawa na serilali ya Afrika Kusini pia imetangaza kuwa zaidi ya watu 900 wamerudi kwa hiari kwenye nchi zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni