Shirika la umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao.
Wakati huo huo wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.
Shirika hilo la UNHCR linasema kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia. Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni