Jumamosi, 25 Aprili 2015

Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Nepal

Majengo yaliyoharibiwa Nepal



Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo magharibi mwa Nepal.
Shirika la utafiti la Marekani lilisema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.5 lilikumba aneo lililo umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara, magharini mwa mji mkuu Kathmandu.
Kuna ripoti za uharibifu ya majengo na idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa haijulikani.
 Mitetemeko midogo ilisikika pia umbali wa hadi mji wa New Delhi na miji mingine kusini mwa India.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni