![]() |
Ryan Giggs na Louis Van Gaal |
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal anaamini kwamba klabu hiyo itamuajiri Ryan Giggs kama mrithi wake.
Giggs mwenye umri wa miaka 41 alisimamia mechi nne msimu uliopita baada ya aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes kupigwa kalamu,kabla ya yeye kupewa kazi ya kuwa msaidizi wa Van Gaal.
Van Gaal ambaye atafikisha miaka 63 anakamilisha msimu wake wa kwanza kama kocha wa Man United na kandarasi yake inamalizika mwaka 2017.
Alipoulizwa kuhusu Giggs,kocha huyo aliiambia runinga ya klabu hiyo kwamba anatumai kwamba ndiye atakayemrithi.
Giggs alisema kwamba alifurahi sana alipopewa jukumu la kuisimamia klabu hiyo baada ya Moyes kupigwa kalamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni