Jumatano, 1 Aprili 2015

Chelsea yamwinda Theo Walcot

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot anawindwa na wasajili wa Chelsea

Kilabu ya Chelsea inaiangazia kwa karibu hali ya kandarasi ya mchezaji wa Chelsea Theo walcot katika kilabu ya Arsenal na huenda ikamsajili iwapo atakuwa huru mwishoni mwa msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza atakuwa amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na hadi kufikia sasa hajapewa mkataba mpya na Arsenal.
Chelsea walianza kumfuatilia Walcot aliposalia na miezi 12 ya kandarasi yake miaka mitatu iliopita kabla ya kutia sahihi mkataba mpya katika uga wa Emirates.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni