![]() |
Patrick Viera |
Patrick Viera anaungwa mkono na wachezaji wengi wa klabu ya Manchester City kumrithi Manuel Pellegrini iwapo klabu hiyo itamfuta kazi mkufunzi huyo ambaye ameshindwa kuimarisha matokeo ya kilabu yake.
Maisha ya Pellegrini katika kilabu hiyo ya Etihad yanaangaziwa kufuatia msururu mbaya wa matokeo.
Vieira atakuwa miongoni mwa wanaotazamiwa kumrithi Pellegrini iwapo bodi ya klabu hiyo itaamua kumpiga kalamu kocha huyo.
Wachezaji wengi wanataka raia huyo wa Ufaransa kupewa uongozi wa kilabu hiyo iwapo Pellegrini atang'atuliwa.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal anaheshimiwa sana na wachezaji wa klabu hiyo.
Vilevile kazi yake nzuri na kikosi cha vijana chipukizi katika klabu hiyo imeonekana na wachezaji hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni