Simiyu
yajipanga kurasimisha kazi za sanaa, utamaduni kutengeneza ajira kwa
wananchi ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa sambamba
kukuza utamaduni wetu.
Aidha umekusudia kuandaa utaratibu kwa
kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha
Sanaa Bagamoyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuona namna
ambavyo kazi za sanaa,utamaduni na michezo zinazofanyika mkoa wa Simiyu
kufanywa kibiashara ili kutanua wigo wa ajira na kuvutia watalii.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu Tamasha la “Simiyu Jambo Festival”
litakalohusisha mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili ambalo litafanyika
Agosti 06, 2017 uwanja wa halmashauri ya mji Bariadi huku mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Tulia
Ackson
Mtaka
alisema vikundi vya sanaa na utamaduni vya Mkoa wa Simiyu vitapewa mafunzo ya
namna ya kufanya kazi zao kitaalam na kazi zao zitarasimishwa , ziweze kuuzika
ndani na nje ya mkoa ili kila mwenye kipaji atambulike.
“tunaamini
Kipaji cha mtu ni biashara na kipaji ni ajira vijana wangi Mkoani hapa
wanafanya vizuri katika mchezo wa baiskeli tutafanya utaratibu wa kupewa
mafunzo ya kuwaimarisha zaidi katika mchezo huo, ili Mkoa ufikie hatua ya kutoa
wawakilishi kwenye mashindano makubwa ya mbio za baiskeli mfano mashindano Jumuiya ya Madola na Olimpiki”.alisema Mtaka
na kuongeza kuwa:
“tungehitaji
sisi kama mkoa tufike mahali ambapo kazi za sanaa na utamaduni ndani ya mkoa wetu zifanywe kibiashara…wakati watalii
wanapotembelea hifadhi za Taifa wasiishie kupiga picha na kuangalia wanyama,
tungehitahiji vikundi vyetu vya sanaa na utamaduni viuze kazi zao huko”.
.
.
Kwa upande wake
mwenyekiti
wa Chama cha baiskeli Mkoa wa
Simiyu Joseph Paul amesema mashindano hayo ni chachu ya kujenga udugu,
ushirikiano sambamba na kuongeza ajira huku akiishukuru kampuni ya Jambo Food
Product ya mkoani Shinyanga kudhamini mashindano hayo ya Mbio za baiskeli
ambayo yatahusisha makundi matatu; kilometa 200 kwa wanaume, Kilometa 80
wanawake na Kilometa 5 kwa watu wenye Ulemavu.
“tumejipanga
viziri tumeshapata zaidi ya washiriki 150 katika mikoa ya Simiyu,Geita,Mwanza,
Shinyanga na Arusha na kila mshiriki lazima ajaze fomu ya ushiriki
inayopatikana kwa shilingi 5000 “alisema mwenyekiti huyo
Anthony
Paul ni meneja wa masoko wa kampuni ya Jambo Food Product amesema Kampuni
hiyo ambayo ni wadhamini wakuu wa
Mashindano hayo wamejipanga kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo Pikipiki
itakayotolewa kwa mshindi wa Kwanza mbio za wanaume na fedha taslimu zaidi ya
shilingi milioni 8 zitashindaniwa.
“mshindi
wa kwanza kwa wanaume atazawadiwa pikipiki
upande wa wanawake laki tano upande wa watu wenye ulemavu shs laki
mbili na upande wa ngoma(wagika,wagalu )kila moja likipata shs milioni moja”alisema
Paul
Na ANITA BALINGILAKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni