Jumanne, 4 Julai 2017

MIRADI YA BILIONI 8 KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU SIMIYU

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe.Anthony Mtaka akipokea Mwenge wa Uhuru  kutoka kwa moja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa leo katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.


MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake juzi mkoani  Simiyu na utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya shilingi bilioni  8,450,841,622

Katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka
wa 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umetekeleza  Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”

Aidha Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea  na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji, viwanda, Vijana na wanawake,Miundombinu ya barabara, kilimo, maliasili, ushirika na utawala bora.  

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.Amour Hamad Amour  katika kijiji cha Bukundi kilichopo wilaya Meatu ambapo mwenge umepokelewa ukitokea mkoani singida.

“ ndani ya mkoa wa simiyu kuna viwanda viwili maswa chaki na meatu milk ambavyo vitasaidia ajira kwa vijana huku halmashauri zingine zikiwa kwenye upembuzi yakinifu kufanikisha ujenzi wa viwanda”alisema Mtaka

 Akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu  kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour ameipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za mama na mtoto huku akiwataka kulitunza  jengo hilo  .
“miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito ni pamoja na huu....  nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani njoo hapa majumbani mnahatarisha maisha yenu, alisema kiongozi huyo.

Mwenge wa uhuru unatarajia kupitia halmashauri sita ambazo ni meatu, itilima, bariadi tc, bariadi dc, busega , maswa na july 10 utakabidhiwa mkoani shinyanga
 
 Mwenge wa Uhuru  ukipelekwa eneo la mradi wa maji katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu kwa ajili ya kufungua mradi huo.
 
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour akifungua  jengo la Kitega uchumi  la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Walimu wa  Wilaya ya Meatu KINYAKI SACCOS.

Na ANITA BALINGILAKI SIMIYU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni