Hofu ilietanda kwa wakazi wa kijiji
cha mwaholo kata ya mwamanenge wilayani
maswa Mkoani Simiyu, baada ya tukio la mtoto kushambiliwa hadi kufa na mnyama aina ya fisi
kijiji hapo..
Tukio hilo ni la kwanza kutokea
kijijini hapo huku baadhi ya wananchi
wakisema lina uhusiano na imani za kishirikina na wengine wakisema
halina uhusiano wowote na imani hiyo.
“huyu fisi atakuwa ameasi na
kufukuzwa na wenzake au yaweza kuwa ana ugonjwa maana wakufugwa haogopi watu na
avizii porini” alisema mmoja wa wananchi
“haiwezekani fisi wa saa kumi na
mbili bado kweupe hivi mh…kuna namna” alisema mmoja wa wanawake waliokuwa eneo
la tukio
Tukio hilo limetokea juzi majira ya
saa kumi na mbili jioni wakati mtoto huyo ambaye jina lake halikufahamika mara
moja jinsi ya kiume (6) alipokuwa akikata kuni alizotumwa na mama yake akiwa na
mwenzake ndipo fisi alipotokea na
kuwakimbiza na kumkamata mtoto huyo na kukimbia nae .
Mtoto aliyenusurika ambaye jina lake
alikufahamika mara moja alikimbia nyumbani kutoa taarifa na jitihada za
kumtafuta zilianza bila mafanikio mpaka kesho yake ndipo mwili ulipatikana
ukiwa umebakizwa fuvu na mbavu.
Katika eneo la tukio baadhi ya wananchi
wanasema hali kwa sasa ni shwari
kutokana na kupata msaada wa kutosha kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya maswa
huku wakiiomba serikali kuendelea kuwasaidia kuwasaka wanyama hao hatari
wasilete madhara zaidi kwa watu na mifugo.
“ tunaishukuru ofisi ya mkuu wa
wilaya kwa ushirikiano iliyotupa japo mtoto kabakizwa fuvu ila fisi kauliwa alisema
mmoja wa wananchi ambaye akutaka kutaja jina lake na kuongeza kuwa nashanga
mwananenge fisi wapo ila hawana historia ya kula mtu sasa huyu fisi ni fisi
fisi au mtu”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya dr self
shekhalage alisema kuwa alipata taarifa za kuwepo kwa hali hivyo akalazimika kufika
eneo la tukio sambamba na kuitisha kikao
cha kamati ya ulinzi na usalama ili kuweza kuweka mikakati ya kupambana na
wanyama hao.
“tumefika eneo la tukio na
kufanikiwa kumuua fisi huyo na tayari nilishatoa maelekezo ofisi ya maliasili
kuhakikisha wanazunguka eneo lote kubaini kama wapo fisi wengine na kujua ni
wapi walipotoka kama ni kwenye hifadhi taratibu za kuwarudisha zifanyike mara
moja” alisema mkuu huyo. Na kuongeza kuwa tumesimamia mazishi ya mtoto huyo na
ninawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha hapa.”
Hata hivyo amewataka wazazi na
walezi kutowaacha watoto peke yao porini wakichunga, kucheza au kutafuta kuni
ili kuwaepusha na hatari ya wanyama hao.
Na ANITA BALINGILAKI MASWA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni