Mkoa wa SIMIYU unatarajia kujenga kiwanda kikubwa na chakisasa cha chaki chenye teknolojia mpya katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambacho kitasaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa
SIMIYU, ANTHONY MTAKA katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya
utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ya MASWA na kufafanua mikakati ya mkoa
katika kutekeleza azma ya serikali ya viwanda.
Tangu kuingia madarakani Serikali ya Awamu ya TANO moja ya mambo iliyoyapa kipaumbele katika utekelezaji wa ahadi zake kwa watanzania ni kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda na kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025.
Katika kuunga mkono azma hiyo ya serikali tayari mkoa
wa simiyu umeanza jitihada mbalimbali za kutekeleza azma hiyo ambayo itatoa fursa ya ajira kwa watanzania wote.
Aidha mh mtaka amesema kwa kuendeleza mikakati hiyo
Wilaya ya MASWA tayari imeshaanza kujenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha chaki
na tayari Shilingi Milioni HAMSINI zimeshatolewa kwa ajili ya upembuzi
yakinifu.
mh MTAKA ameziagiza halmashauri zote
za mkoa hapa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuachana na tabia ya
kuwatoza ushuru wafanyabiashara wadogo pamoja na wakulima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya MASWA Dokta FREDRICK SAGAMIKO amesema wameshaanza
mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya ngozi chini ya ubia
wa wajasiriamali wa Kijiji cha SENANI, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo -SUA
na Chuo cha Teknolojia -DIT ambacho kitakamilika Julai mwaka huu.
NA ANITA BALINGILAKI
===
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni