Jumamosi, 27 Mei 2017

AMREF KUJENGEA UWEZO WATOA HUDUMA




AMREF kwa kushirikiana na wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee,na watoto  wametekeleza mradi wa jenga uwezo kwa watoa huduma za afya  ngazi za jamii kuongeza nguvu kwenye sekta ya afya hususan kitengo cha afya ya uzazi.

Mradi huo umetekelezwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo katavi na shinyanga  huku mkoa wa simiyu ukiwa wa mfano na jumla ya watendaji wa kata na vijiji  370 wamejengewa  uwezo ili kusaidia kutekeleza sera kwani wao ndo wapo karibu na wananchi  awali  elimu hiyo ilitolewa kwa wakurugenzi watendaji ,maafisa utumishi na wagaga wakuu wa halmashauri za wilaya zote mkoani hapo.

Akiongea kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa kata na vijiji mkuu wa mkoa wa simiyu Antony Mtaka amewataka viongozi kuthibiti ndagashida ili watoa huduma waweze kufanya kazi zao kwa umakini na kutoa utambuilisho wa kutosha kupitia mkutano wa kijiji  kuhusu ujio wa watoa huduma ili jamii iweze kuwatambua na kutoa ushirikiano wa kutosha.
“ole wake atakayeleta habari za ndagashida atakiona cha moto …watendaji simamieni na mtoe utambulisho wa kutosha ili ushirikiano uwepo alisema” mkuu huyo

Mtaka amewaomba AMREF isaidie kutoa ajira kwa watu waliopata mafunzo huku akiwaomba wadau kusaidia vifaa ili watoa huduma wanapoenda huko wawe wamejitoleza  kutoa huduma ngazi ya jamii.
Aidha kwa upande wake dr Ama Kasangala afisa mpango wa huduma za afya ngazi ya jamii kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee,na watoto  amesema wapo kwaajili ya kutoa elimu kuhusiana na sera ya afya hasahasa sera ya afya ya mwaka 2014 ambayo imezungumzia afya ya msingi ngazi ya jamii .

Hata hivyo dr Kasangala ameongeza kuwa lengo la watoa huduma  ni kuzuia na sio kutibu na watasaidia   huduma  za afya ndani ya familia / kaya hivyo watakuwa kiungo kati ya jamiii na zahanati na  kupunguza msongamano wa wagonjwa.
“tunampango wa kuwafikia watu wote kwa uharaka zaidi na hasa maeneo ambayo hayana  vituo vya afya 
kwa ukaribu na ndo maana tumeongea na watendaji wa kata na vijiji wale ndo watendaji ili watusaidie kutekeleza sera”alisema dr Kasangala
NA ANITA BALINGILAKI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni