Serikali wilayani bariadi mkoani simiyu kuunda sheria ndogo za uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kulinda uoto wa asili usipotee.
Sheria hizo zitahusisha wakata miti ovyo watupa taka ovyo
hususan taka ngumu ikiwemo mifuko ya plasitiki
chupa za plasitiki na mifugo inayozurura ovyo.
Hatua hiyo ilikuja kufatia benki ya CRDB tawi la bariadi
kuonyesha njia kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa ,jeshi la polisi kuanzisha
kampeni ya upandaji miti ya vivuli kando
ya barabara kuu ya bariadi lamadi,bariadi maswa .
Akiongoza zoezi hilo kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi
la polisi Boniventura Mushongi alisema kuwa ni vema jamii ikajua umuhimu wa
miti kwenye mazingira huku akisisitiza kuwa ni vema zoezi hilo likawa endelevu
“Uchumi wa bariadi unategemea kilimo na kilimo ni mvua na
mvua ni uhifadhi mzuri wa mazingira hivyo basi…tukipanda miti na kuitunza mvua
itanyesha sana tutalima sana na kuvuna sana” alisema Mshongi.
Mathias Mkumbo ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji
bariadi alisema sheria hizo zitawabana wale wote wanaokiuka
taratibu za halmashauri na
kimazingira huku akiwashukuru benki ya CRDB tawi la bariadi na kuahidi kutoa ushirikiano wa kuitunza miti hiyo .
“Tuendelee kutunza miti tutie moyo watu wanaotusaidia ili kuendelea kuhifadhi wenzetu CRDB wameonyesha njia upandaji miti 60 ni mfano wa
kuigwa ” alisema mkumbo
Naye meneja wa CRDB Samwel Kishosha alisema kuwa lazima
benki irudishe fadhira kwa jamii huku akiongeza kuwa lengo la zoezi hilo ni
kufanya mazingira ya mkoa wa Simiyu kuwa na uoto wa asili huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa
wingi kupanda miti katika maeneo yao ,taasisi pamoja na ofisi.
“hii itakuwa njia mojawapo ya kupambana na changamoto ya ukame simiyu, mabadiliko ya tabia nchi”, alisema meneja huyo.
NA ANITA BALINGILAKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni