![]() |
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Onesmo Lyanga akiwa na baadhi ya maaskari tayari kuanza kazi ya kuteketeza bangi |
Jeshi la
polisi Mkoani Simiyu limefanikiwa kukamata tani 2 za bangi na kuteketeza kwa
moto zaidi ya hekari 5 katika kijiji cha Ihusi kilichopo jirani na hifadhi ya
Taifa ya Serengeti na pori la akiba la Maswa.
Akizungumza katika oparesheni
iliyofanyika jana katika kijiji cha
ihusi Kamanda wa polisi Mkoa wa Simiyu Onesmo Lyanga alisema kuwa
wameamua kufanya msako huo katika maeneo hayo kutokana na
kupata taarifa za kukithiri kwa kilimo cha bangi.
Kamanda
Lyanga amesema kuwa oparesheni hiyo ni endelevu kwa mkoa huo ili kubaini vyanzo
vya madawa ya kulevya na kuyateketeza kwa lengo la kuokoa kundi la vijana
ambalo limeathiriwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake
mkuu wa upelelezi mkoa wa simiyu Jonathan Shana amesema jeshi hilo
limebaini mashamba zaidi ya kumi na mbili kijijini hapo hivyo oparesheni hiyo
inaendelea.
Hata hivyo jeshi
hilo linawashikilia watu 7 kwa kujihusisha na kilimo cha bangi akiwemo mwenyekiti wa kijiji kwa kushindwa kutoa taarifa yakuwepo kwa mashamba hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni