![]() |
moja ya nyumba iliyobomolewa na mvua |
Mvua za masika zinazoendelea kunyesha ,zimeleta madhara katika kata ya Njoro manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo kaya zaidi ya 100 nyumba zao zimeharibiwa na mafuriko yaliyotokana na mvua hiyo huku kaya 11 nyumba zao zikiwa zimebomoka sambamba na kuharibu vitu mbalimbali zikiwemo samani na vyakula.
Joseph Shio ni afisa mtendaji wa kata ya njoro .amesema mafuriko hayo yametokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha,ambapo amesema kukosekana kwa miundombinu mizuri ya kusafirisha maji,yanayotoka maeneo ya milimani katika manispaa ya moshi ndio chanza kwasababu maji hayo huelekea kata ya njoro ambayo iko eneo la bondeni.
Akizungumza wakati wa kukambidhi msaada wa vyakula ,ikiwemo ,unga wa sembe,mchele ,sukari ,na maharage ,viliyotolewa na jumuiya ya Khoja Shia Jamaat ya Mjini Moshi ,ambao pia wametoa msaada wa matibabu kwa wahanga wa mafuriko hayo mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga amewataka viongozi wa kata kusimamia vyema ugawaji wa msaada huo.
Diwani wa kata ya Njoro Bw Jomba Koi ,amesema wamesha peleka bajeti halmashauri ya manispaa ya Moshi ,ya ujenzi wa mtaro kubwa, wenye urefu wa mita 600 ,utakaojengwa kwa awamu mbili ,kwaajili ya kusafirisha maji yatokanayo na mvua ,pamoja na yale yanauyozalishwa kutoka katika manispaa hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni