Alhamisi, 14 Aprili 2016

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAMEUAWA


askari wakiimarisha ulinzi


Askari polisi wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wamewaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika tukio la mapambano ya kurushiana risasi wakati wakizima jaribu la kupora fedha katika duka la mfanyabiashara mmoja, Emmanuel Mkumbo, mjini Kahama katika tukio hilo mfanyabiashara huyo pamoja na mtu mmoja mpita njia waliuwawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao.

Tukio hilo limedumu kwa takribani saa tatu kuanzia majira ya 12:00 jioni hadi saa 20:00 usiku inadaiwa majambazi hao wapato watano walifika katika duka hilo na kumtaka mmiliki huyo wa Duka kuwapatia fedha lakini aligomba ndipo majambazi hao walimpiga risasi kifuani pamoja na mpita njia mmoja aliyefahamika kwa jina la Selemani Shaban ambapo baada ya kusikika milio ya risasi, askari polisi waliojidhatiti kwa silaha walifika eneo la tukio na kupambana kiume kuzima tukio hilo na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu huku wawili kati yao wakitoroka na kwamba majeruhi wote wawili waliopigwa risasi na majambazi hao, walifariki dunia wakati wakipatia matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Katika tukio hilo Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Bunduki mbili aina ya SMG na UZIGAN, magazine 3, kisu na mkanda vya kijeshi na pikipiki mbili aina san LG.

Jeshi la polisi mkoani hapa linawasaka majambazi hao ili kuwachukulia hatua za kisheria

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni