![]() |
ALIYEKUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA BW TRANSIAS B KAGENZI ENZI ZA UHAI WAKE AKIWA OFISINI KWAKE |
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Kassimu
Majaliwa ameahirisha ziara yake ya kikazi
iliyokuwa ifanyike kesho wilayani maswa mkoani Simiyu.
Mh Majaliwa ameahirisha ziara hiyo kutokana na kifo cha
aliyekuwa mkurugenzi mtandaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa bw Transis B
Kagenzi aliyefariki usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa msemaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa bw Masanja Shilabu ambaye ni afisa kilimo wa
wilaya ya Maswa amesema marehemu alikuwa akifanya mazoezi ya
asubuhi baada ya kujihisi vibaya
alipelekwa hospitali ya wilaya ya Maswa.
Hata hivyo amesema kuwa baada ya hali kubadilika alipelekwa hospitali
ya rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza kwa matibabu zaidi na umauti ulimkuta
wakati akiendelea na matibabu
Aidha mh Waziri mkuu anaendelea na ziara yake
wilayani Meatu na kesho atahudhuria ibada ya kuuga mwili wa marehemu
itakayofanyika saa 3:00 asubuhi kwenye
ukumbi mkubwa wa halmashauri ya wilaya ya Maswa,mara baada ya kuaga mwili
utapelekwa wilayani Karagwe mkoani Kagera kwaajili ya mazishi
Tayari mwili wa marehemu umeshawasili wilayani maswa na
kuhifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya maswa , huku taratibu za mazishi
zikiendelea nyumbani kwake mtaa wa uzunguni Maswa.
"BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIIMIDIWE"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni