Jumatano, 6 Mei 2015

Uchaguzi Mkuu Uingereza kufanyika kesho

Wagombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza 
Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.

Waziri Mkuu David Cameron ameaahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati  kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ameaahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi" na Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ameaahidi hali ya utulivu.

Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni