Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde.
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema kuwa wanafunzi
wanaofanya mtihani wa kidato cha sita na ualimu, walifanya mtihani huo
jana licha ya kuwapo kwa baadhi ya waliochelewa kufika katika chumba cha
mtihani kutokana na mgomo wa mabasi juzi na jana.
Baraza hilo lilisema kuwa pamoja na kuwapo kwa changamoto ya
usafiri, watainiwa hao walianza mtihani huo Mei 4, wanatarajiwa
kumaliza Mei 27 mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde alisema
jana jijini Dar es Salaam kuwa jumla ya watahiniwa 40, 758 walisajiliwa
kufanya mtihani mwaka huu kati yao watahiniwa wa shule ni 35,385 na
ualimu ni 19,924.
“Tangu mtihani ulipoanza, mitihani 12 ya kidato cha sita na
stashahada ya ualimu hadi jana, imefanyika kwa utulivu na amani katika
mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar,” alisema Dk. Msonde.
Alisema pamoja na kuanza mtihani huo kukiwa na mgomo wa mabasi ya
daladala, watahiniwa walifika katoka vituo vya na kufanya mitihani kwa
mujibu wa ratiba ilivyopangwa.
Alisema Necta ilipoona kuna mgomo ilitoa taarifa kwa wasimamizi wasiwazuie wanafunzi watakaochelewa na kufidia muda waliochelewa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni