Jumamosi, 2 Septemba 2017

DC MASWA:TATIZO LA MAJI KUTATULIWA NDANI YA WIKI MBILI



Aliyesimama ni mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya maswa dkt Self shekalaghe akiongea na waislamu kwenye baraza la Eid El Hajj

Wakazi wa wilaya ya maswa wanatarajia kuondokana na kero ya maji iliyoukumba wilaya hiyo kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kukauka kwa bwawa la new sola ambalo lilikuwa likitegemewa wilayani hapo.
Aidha serikali imejipanga ndani ya wiki mbili zijazo  kumaliza tatizo hilo kwa kuweka mabomba kwenye visima ili maji yawafikie wananchi kwa ukaribu kupunguza tatizo hilo.
Bwawa hilo ndicho chanzo kikuu cha maji katika mji huo kwenye vijiji vipatavyo 11 huku likitegemewa na wakazi wapatao 78,190 na mifugo zaidi ya 400,000.
 Hayo yalisemwa na mgeni rasmi ambaye mkuu wa wilaya hiyo dkt self shekalaghe wakati akiongea na waislam kwenye baraza la eid el haji lililofanyika kwenye msikiti wa baraza kuu wilaya hapo.
“kuhusu tatizo la maji ndani ya wiki mbili maji yatapatikana tumejipanga kuhakikisha tatizo hilo linakwisha alisema dkt  shekalaghe na kuongeza kuwa:

“jamani maji tunayoyapata sasa japo ni meupe ila si safi na salama hivyo jitahidini kuchemsha msije pata magonjwa ya matumbo”

Bwawa hilo ndicho chanzo kikuu cha maji katika mji huo kwenye na vijiji vipatavyo 11 linalotegemewa na wakazi wapatao 78,190 na mifugo zaidi ya 400,000.

Alisema moja ya  sababu  zinazosababisha bwawa hilo
kukauka  ni pamoja na msimu uliopita kutokuwa na mvua za
kutosha  ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa hali hiyo sambamba na
baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya eneo
la bwawa hilo na kwenye vyanzo vinavoingiza maji katika bwawa  la New
Sola.

“Mwaka jana kutokana na mvua kutokuwa nyingi bwawa la New Sola
halikupata maji ya kutosha pamoja na hayo lakini ukiangalia kandokando
ya bwawa na hata kwenye vyanzo vyake vinavyoingiza maji kuna watu
wanalima mashamba,wanakata miti hovyo na wengine hata kudiriki
kuingiza mifugo yako kunywesha katika bwawa haya yote ndiyo
yamesababisha hali hii ya kujaa tope na kupungua kwa kina,”


Hata hivyo ,Dkt Shekalaghe alisema tayari  hatua za dharura za zimeanza kuchukuliwa na maji yataanza kupatikana ndani ya wiki mbili zijazo 


Katika hatua nyingine amewataka waislamu wilayani hapo  kudumisha umoja na amani huku viongozi wa dini hiyo wakitakiwa kuwa waadilifu na watenda haki kwa wote
 
Baadhi ya waislamu wakiwa kwenye baraza la Eid El Hajj


watoto wa madrasa wakisoma QURAN kwenye baraza la Eid El Hajj


Baadhi ya waislamu wakiwa kwenye baraza la Eid El Hajj


 

Baadhi ya waislamu wakiwa kwenye baraza la Eid El Hajj

Na ANITA BALINGILAKI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni