Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano mjini Bariadi |
NAIBU sipika wa bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony
Mtaka kwa utekelezaji wa agizo la ujenzi wa viwanda kwa asilimia 95.
Pongezi hizo zinaendana na
utekelezaji wa kauli mbiu ya Rais wa Tanzania Dk Joseph Pombe Magufuli
katika kampeni zake alipokuwa akiwaamba watanzania kuweza kumchagua ili aweze
kuwatumikia kama Rais wao,lakini aliahidi kuwa moja ya vitu ambavyo anataka
kuviona katika nchi ya Tanzania ni uwepo wa utitili wa viwanda katika kila mkoa
.
Maneno hayo ameyasema jana alipokuwa
akishiriki katika tamasha (Simiyu jambo Festival) lililojuisha michezo
mbalimbali ya asili ikiwemo uendeshaji wa baiskel kwa wanawake na wanaume nawatu
wenye uwalemavu,mgoma za asili za wagika
na wagalu,michezo ya nyoka na michezo ya fisi.
Dk Tulia alisema kuwa Simiyu imekuwa
miongoni mwa mikoa ya mfano katika nchi yetu kwa utekelezaji wa kauli mbiu ya
Tanzania ya viwanda,kwani mpaka sasa simiyu inaviwanda zaidi ya vitano na vyote
vikiwa tayari vinafanya kazi na kuongeza ajira kwa vijana wa mkoa humo.
“Nimependa kauli mbiu ya mkoa wa
Simiyu isemayo wilaya moja bidhaa moja hivyo hii inamanisha ni jinsi gani mkuu
wa mkoa huu alivyo na ubunifu na ushawishi wa hali ya juu kwa wananchi wake wa
Simiyu” Alisema
Aidha alisema kuwa atahakikisha
anakuja kujifunza kupitia mkoa wa Simiyu ili naye akafanye ya simiyu katika
mkoa wake wa mbeya ili aweze kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana wa mkoa
wake kama vile ajira zilivyotengenezwa katika mkoa wa Simiyu.
Kwa niaba ya serikali tunahakikisha
mkoa wa simiyu unakuwa miongoni kwa mikoa ya kipekee katika ukanda wa ziwa na
hii ni kutokana na utekelezaji wa hali ya juu ya ujenzi wa viwanda.
Mbali na hilo amewapongeza wabunge
wa mkoa wa simiyu kwa umoja na upendo wao katika ushirikiano wao bungeni na
hata katika mkoa kwani kila mbunge wa simiyu kwenye jimbo lake kuna kiwanda hii
inaonyesha ni jinsi gani wabunge na serikali wanavyoshirikiana kwa ukaribu ili
kuwatumikia watanzania wa hali ya chini.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa
Simiyu Anthony Mtaka amempongeza naibu spika kwa ujio wake katika mkoa wa
Simiyu na kuweza kujionea mambo mengi yaliyopo katika mkoa huo.
“Sisi kama mkoa mbali na
kushughulika na viwanda pia tumeanza mikakati mingine ya kuwasaidia vijana wote
walio na vipaji katika mkoa huo kujisajiri”alisema mtaka na kuongeza kuwa:
“viwanda ambavyo vipo simiyu kiwanda cha chaki Maswa,Maziwa Meatu,Busega
Tomato na mazao limited,Bariadi Unga.
Na ANITA BALINGILAKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni