Jumatatu, 16 Novemba 2015

SHULE YA MSINGI IGWATA YAFANYA VIZURI MIAKA SABA MFULULIZO WILAYANI MASWA

                       BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IGWATA

Ufaulu mdogo kwa watahiniwa wa darasa la saba mkoani Simiyu umekuwa ukisababishwa na utoro  kwa baadhi ya wanafunzi na shule ya msingi igwata kwa kulitambua hilo imefanya jitihada za makusudi kikomesha tatizo hilo ili kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo.
Hayo yameelezwa na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu Julius Nestory ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya kuipongeza shule ya msingi Igwata iliyofanyika shuleni hapo.

Hafla ilihudhuriwa na afisa elimu wa mkoa na wilaya, kaimu RPC, waratibu kata ,walimu wakuu wa shule za msingi ,wajumbe wa kamati ya shule pamoja na baadhi ya wazazi.
kushoto ni afisa limu mkoa Julius Nestory kaikati kaimu RPC Audax Selestini na kulia ni afisa elimu wa wilaya Mabeyo Bujimu  

 kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya shule Joseph Mashala katlkati ni afisa elimu mkoa Julius Nestory kulia kaimu RPC Audax Selestini
                                     Baadhi ya wakuu wa shule ,wanakamati na wazazi

Afisa elimu huyo amesema shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo zimeuinua mkoa wa Simiyu kwa ufaulu mzuri kutoka katika  nafasi ya 22 mwaka jana hadi kufikia nafasi ya 16 kwa mwaka 2015.
Shule ya msingi Igwata ilikuwa ikifanya vizuri kwa miaka 7 mfululizo Mwaka huu ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa nafasi ya pili nafasi ya kwanza kimkoa ikishikiliwa na shule ya alliance iliopo wilayani bariadi  huku kitaifa ikiwa ya 101.
“Ninawapongeza sana kwa kufanya vizuri kwenye masomo yenu kwa zawadi ya gunia moja la mahindi bado jitihada za makusudi zinahitajika.”alisema Julius

Hata hivyo alisema Wilaya ya Maswa ina shule 120 lakini hazifanyi vizuri hivyo ni lazima utoro mashuleni ukomeshwe.
“Nitajitahidi kushirikiana na walimu wangu pamoja na jeshi la polisi ili tukomeshe utoro, watoto wasome” alisema Nestory

Shule ya msingi igwata mwaka juzi ilishika nafasi ya pili kimkoa na kitaifa ilikuwa ya 101,mwaka jana ilikuwa ya tatu kimkoa na kitaifa ilikuwa ya 232 na ipo kilometa 70 kutoka maswa mjini.
 Wanafunzi hupata uji na chakula cha mchana hali inayowafanya kutumia muda wao vizuri kujisomea badala ya kurudi nyumbani kutafuta chakula.

wanafunzi wakipata chakula cha mchana

Kwa upande wa afisa elimu wa shule za msingi wa wilaya  Mabeyo Bujimu alisema walianzisha mfumo wa kuwatambua na kuwafikia wahitimu wa 2016 kabla ya mwaka kuanza.  

Naye mwalimu mkuu wa Igwata James Mayunga alisema shule yake inafanya vizuri kila mwaka kutokana na kamati nzuri ya shule pamoja na ushirikiano wa walimu.
Pia aliongeza kuwa wanafunzi wanapata uji saa 4:00 asubuhi na chakula cha mchana kila siku bila kusuasua toka mwaka mwaka 2010 ambacho kinatokana na michango ya wazazi na shule hiyo pia inamashamba.
“Utoro umepungua kutokana na chakula tunachotoa kwa wanafunzi wetu ndio maana tunafanya vizuri kitaaluma” alisema Mayunga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni