![]() |
Zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo baya zaidi la ardhi, katika kipindi cha muongo mmoja. |
Makundi ya uokoaji yanajikakamua kufikia maeneo ya vijijini zaidi Kaskazini mwa Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan, ilikuwaokoa watu wanodhaniwa kuwa wameathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo hilo hapo jana.
Kufikia sasa zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo baya zaidi la ardhi, katika kipindi cha muongo mmoja kuwahi kukumba mataifa hayo yaliyoko bara Asia.

Zaidi ya watu elfu mbili wamejeruhiwa.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Afghanistan, yanadhibitiwa na wanamgambo wa Taliban, na inakuwa vigumu mno kwa maafisa wa serikali na waokoaji kuyafikia ili kutoa usaidizi.
Maafa makubwa zaidi yameripotiwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan.

Vyombo vya dola huko vimeripoti kuwa takriban watu 214 wamepoteza maisha.
Hali ni mbaya mno katika maeneo yenye milima na mabonde ambako kumeripotiwa maporomoko ya ardhi.

Aidha katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa utawala umetangaza kuwa watu 179 walipoteza maisha yao huku wengine 1,800 wakijeruhiwa.
Kitovu cha tetemeko hilo lenye nguvu ya 7.5 kwenye vipimo vya Richter kilikuwa maeneo yenye milima mingi ya Hindu Kush, kilomita 45 kusini magharibi mwa Jarm, Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani imesema.

Nchini Pakistan, vyombo vya habari vilionyesha picha za watu wakikimbia na kutoka kwenye majengo.
Bado hakuna ripoti zozote rasmi kuhusu majeruhi lakini baadhi ya ripoti zinasema watu wanne wamefariki kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni