Jumatatu, 8 Juni 2015

Visa vya MERS vyaongezeka Korea Kusini


Mhudumu wa afya akiwa nje ya hospitali Korea Kusini
Maafisa wa afya nchini Korea kusini wamegundua visa vingine 23 vya ugonjwa uitwao Middle East Respiratory Syndrome - kwa kifupi MERS.
Ukiongezea na visa vya hapo awali, idadi ya watu waliambukizwa ugonjwa wa MERS sasa inafikia 87, huku watu watano wakiwa tayari wamefariki kutokana na ugojwa huo .
Nyingi ya visa vya ugonjwa huo vimegunduliwa kwenye hospitali moja mjini Seol ambapo mgonjwa wa kwanzamwanamke mfanyibiashara, ambaye alizuru Saudi Arabia alitibiwa.
Mlipuko huo wa ugonjwa wa MERS ndio mbaya zaidi kuwai kushuhudiwa nje ya eneo la mashariki ya kati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni