Jumanne, 9 Juni 2015

Salazar akana tuhuma dhidi yake

Kocha wa mchezo wa riadha,Alberto Salazar


Kocha wa mwanariadha Mo Farah, Alberto Salazar amekana shutuma dhidi yake kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni akidai kuwa wanaomshutumu wametoa kauli za uongo dhidi yake.
Salazar anayemfundisha Farah nchini Marekani,amekana tuhuma zilizotolewa na uchunguzi wa BBC katika uchunguzi wake,kuwa alitumia mbinu zisizokubalika.
Hakuna shutuma zozote zinazomgusa Farah kuhusika na matumizi ya dawa hizo.
Uchunguzi wa BBC umedai kuwa Salazar ambaye alikuwa Kocha wa Farah mwaka 2011, alikiuka sheria za kupinga dawa zilizopigwa marufuku michezoni na alimpatia dawa hizo ,bingwa wa mbio za mita 10000 Galen Rupp wa Marekani alipokuwa na umri wa miaka 16 mwaka 2002.
''Nitabainisha na kuwasilisha vielelezo kuhusu jambo hili mapema niwezavyo ili Galen na Mo waweze kuelekeza nguvu zao katika kile wanachokipenda na wamefanya jitihada kubwa kufikia mafanikio hayo ''Salazar aliiambia Guardian.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni