Wazazi wengi wanapuuza dalili za mapema kuwa watoto wao wamenenepa kupita kiasi.
Madaktari wanasema kuwa wazazi wengi hawajui madhara ya afya kwa watoto walionenepa kupita kiasi.
Katika utafiti huo uliowajumuisha zaidi ya familia 2,976 nchini Uingereza ni wazazi 4 pekee waliokuwa na shauku kuwa mtoto wao alikuwa amenenepa kupita kiasi.
Madaktari wenye walikuwa wamewatambua watoto 369 kati yao waliokuwa na kiwango cha juu cha mafuta mwilini.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa watoto walionenepa kupita kiasi sasa wamekuwa kawaida tu majumbani.
Watafiti hao wanaonya kuwa hili ni janga kwa afya ya jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni