Jumanne, 31 Machi 2015

Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali




Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan.
Lakini majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo na  mchuano bado ni mkali.
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni