Na ANITA BALINGILAKI , maswa
Jumla ya vikundi 18 jana
vimepokea mkopo wa zaidi ya sh milioni 31 kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya maswa.
kwaajili ya kilimo cha zao la pamba kwa msimu wa kilimo 2017/2018 .
Vikundi hivyo vimepewa mkopo huo baada ya kukidhi vigezo vya
kukopesheka, jumla ya sh milioni 22,630,500 zimetolewa kwenye vikundi 14 vya wanawake huku vikundi vinne vya vijana vikikopeshwa sh milioni 6,556,500 na
kufanya jumla kuwa sh milioni 31,725,000
Mkopo huu utakuwa kwa kipindi kimoja cha msimu wa
kilimo wa 2017/2018
na utatozwa riba ya 10% kwa wanawake na 15% kwa vijana na vikundi hivyo
vinatarajia kulima kuanzia ekari 2 mpaka ekari 51.
Wilaya ya Maswa ina jumla ya vikundi vya wanawake 323 vyenye
jumla ya wanachama 6,128 na vikundi vya vijana 263 vyenye jumla ya wanachama 2,757
kati ya hao wanaume 1,810 na wanawake 947.
Awali uchambuzi wa maombi ulibaini jumla ya vikundi 205 kati
ya 88 vya vijana na 117 vya wanawake
vilikidhi vigezo vilivyowekwa kwenye tangazo
na baada ya uhakiki jumla ya vikundi 25 vya vijana na 31 vya wanawake
vilihakikiwa hali iliyopelekea vikundi 14 vya wanawake na 4 vya vijana kukidhi
vigezo vyote na kupewa mkopo.
Aidha, kwa kipindi cha miaka iliyopita (2013/2014 -2016/2017)wilaya ilitoa mkopo wa Tsh
75,955,000/=mkopo na riba kwa vikundi vya wanawake na sh 105,182,500/=mkopo na
riba kwa vikundi vya vijana ,Tsh 30,162,500 mapato ya ndani na Tsh 75,020,000 zikitoka
wizara ya maendeleo ya vijana habari,utamaduni na michezo.
Akiongea kwa niada ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
maswa afisa maendeleo ya jamii bw lodgers lyimo amesema kuwa kipindi cha
mchakato wa maombi walikutana na changamoto nyingi ikiwemo vikundi vingi vya
vijana vilibainika kudanganya umri huku baadhi ya vikundi vya wanawake
vikigundulika kuwa na wanaume ndani ya vikundi vyao.
Akiongea kabla ya kukabidhi hundi hiyo mwenyekiti wa ccm
wilaya ya maswa Eng Paul Jidayi amesema fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyo
kusudiwa na si vinginevyo ili zilete tija na vikundi vingine vieweze kukopeshwa
kupitia marejesho ya mkopo huo.
“ni vema fedha hizi zikatumike kwa kile kilichokusudiwa si
tusikie mtu kanunulia vipodozi …kaongeza mke na mambo yanayoendana na hayo na
kumbukeni kulipa kwa wakati ili vikundi vingine vikopeshwe”alisema eng Jidayi
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya maswa dr Seif Shekalaghe
aliyekuwa mgeni rasmi Iamesema kuwa mkopo huo umetolewa ni kwaajili ya gharama
za kulimia, viuatilifu ,palizi na mbegu na utatolewa kwa awamu kwa kuzingatia
hatua za kilimo.
“fedha hizo hatutatoa zote zitatoka kwa utaratibu mfano
ukifika muda wa kulima mtapewa ..muda wa
palizi mpaka hatua ya mwisho na hii itasaidia kuratibu kwa ukaribu fedha hizo
maana vikundi vingine vikikabidhiwa zote ni hatari” alisema dkt Shekalaghe
![]() |
Mkuu wa wilaya ya maswa dkt Seif Shekalaghe akiwa na mwenyekiti wa ccm wilaya ya maswa wakimkabidhi mmoja wa wanakikindi mbegu za pamba makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya maswa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni