Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa
na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko.
Shirika la taifa la hifadhi ya jamii NSSF limetoa mkopo
wa bilioni 1.5 kwaajili ya
upanuzi wa kiwanda kikubwa ambacho teknolojia yake haipo afrika mashariki cha
uzalishaji wa chaki wilayani maswa mkoani simiyu.
Mkopo huo una malengo ya kuongeza mtaji wa upanuzi
wa uzalishaji wa chaki ambao utaleta maendeleo kwa wilaya ya maswa, mkoa
na taifa kwa ujumla ,kutanua wigo wa ajira sambamba na kuongeza wanachama wa
mfuko wa NSSF .
Mkuu wa mkoa wa simiyu Antony Mtaka amesema kwenye
halmashauri za mkoa wa simiyu ndani ya miaka mitano zitakuwa za mfano kwenye halmashauri za kipekee kwa kuwa na miradi yake kwa kila moja mfano halmashauri
ya maswa kiwanda cha chaki ,halmashauri ya meatu kiwanda cha maziwa
“Kama halmashauri tunakopa kujenga stendi kwanini tusikope
kujenga viwanda vitakavyotumia malighafi zetu …vitakavyoongeza ajira na kukuza
pato la halmashauri zetu na taifa kwa ujumla wake” alisema Mtaka
Akikabidhi hundi mkurugenzi
mkuu wa shirika la taifa la hifadhi
jamii NSSF prof Godius Kahyarara alisema mkopo huo utaendeleza adhma
ya serikali ya awamu ya tano Tanzania ya
viwanda , kukuza uchumi , kuokoa fedha ambazo zilikuwa zikitumika kuagiza chaki
nje ya nchi na kuongeza wigo wa
mapato kwenye halmashauri.
“kwa vile soko kubwa la bidhaa hii ni serikali yenyewe mradi huu ukisimamiwa vizuri utatoa
fursa ya nchi kutumia rasilimali zake
yenyewe kwa maendeleo ya wananchi
waliowengi”alisema Kahyarara na kuongeza kuwa: jambo la uweklezaji linawezekana na lina faida na tupo bega kwa
bega na serikali kwa uwekezaji wenye faida.
Kwa upande wake mgeni rasmi Waziri wa
kazi,ajira,vijana,sera,bunge na wenye ulemavu Jenista Mhagama alisema mafanikio
ya mradi yanahitaji ushirikiano wa kutosha kwa ngazi zote ,uadilifu ,uzalendo
na weledi wa hali ya juu.
“kila mtu atekeleze kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu ili
kuhakikisha mradi huu unakuwa na kujiendesha kwa faida na fedha yote
iliyowekezwa inarudishwa kwa wakati ili kuleta faida iliyotarajiwa kwani wahenga
walisema kitunze kikutunze”alisema mhagama na kuongeza kuwa:
“Baadhi ya mikoa tayari imeshachukua chaki na kuanza
kuzitumia ikiwemo Zanzibar katoni 2530,
shinyanga katoni 606, geita
katoni 250, tabora katoni 100 ,mwanza katoni 50 na bado kuna oda ya kupeleka chaki Zanzibar zenye thamani ya sh milioni
mia moja arobaini”. 

Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi
Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili
ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka.

Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama( wa pili kushoto) akiangalia kikundi cha ngoma mara mara baada
ya kuwasilisi wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.

Baadhi ya
viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano
ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.

Baadhi ya
viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano
ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
MEANDIKWA NA ANITA BALINGILAKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni