Ijumaa, 3 Julai 2015

DRC yachunguza mauaji ya wawindaji 4

Mauaji ya wawindaji DRC Congo kuchunguzwa

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ,imeanzisha uchunguzi kufuatia vifo vya wawindaji 4 katika eneo la Bandundu takriban kilometa 270 na mji mkuu Kinshasa.
Wawindaji hao walifariki baada ya kula nyama ya swara. Wizara ya afya nchini humo imesema kuwa Kabla ya kufa, watu hao walikuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
Katika mkutuno na vyombo vya habari, waziri wa afya alisema kwamba, kwa muda huu hawezi kuthibitisha wala kukataa kwamba wawindaji hao ambao walifariki baada ya kula nyama hiyo walifariki na virusi ya homa ya ebola .
Kabange Numbi, waziri wa afya ya DRC amesema tayari utafiti utafanyika ili kubainisha chanzo cha vifo hivyo.
Kabange aliongeza kusema kuwa uchunguzi wa aina hiyo umefanyika jijini Bangui, mji mkuu wa jamuhuri ya afrika ya kati baada ya wakongomani watatu kuvuka mto Ubangi, na baada ya uchunguzi wa afya mmoja wao alipatikana na homa ya ebola.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni